Mzee Yusuph: Wakati Umewadia Kurudi Mjini


Mzee Yusuph: Wakati Umewadia Kurudi Mjini
 

Mfalme wa muziki wa Taarab nchini, Mzee Yussuf ameeleza safari yake ya kurejea mjini kama alivyotangaza hapo awali sasa imewadia.

Mzee Yussuf ambaye alijizolea umaarufu mkubwa kwenye muziki huo, kwa sasa anaimba Qaswida lakini hivi karibuni ameeleza kuwa anarudi mjini kwa kile ambacho kinatafsiriwa kuwa huwenda akareja tena kwenye muziki wake wa awali.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, ameweka picha akiwa na Mkali wa Bongo Fleva kwa sasa Diamond Platnumz huku kukiwa na tafsiri mbalimbali kuhusu picha hiyo sambamba na ujumbe aliouandika. Mzee ameeleza...
-
“Wakati umewadia kurudi town nadhani sasa mmeelewa tatizo si ndio maneno sasa yatakwisha haya wale wenye aya mifukoni mwao nwale walokariri ukharamu na uhalali wafunge midomomo yao waniache nirudi mjini NARUDI MJINI SAFINA liko tayari kuondoka ahsanteni kwa kuja FULLDOZ is coming nend kafanye ku subscribe chanel yangu Mzee Yusuph,” ameandika.

Itakumbukwa, Mzee Yusuph ana miaka takribani 6 tangu alipotangaza kuachana na muziki huo na kuanza kuimba Qaswida zenye maudhui ya dini ya kiislam.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad