Nabii Awaonya Wanawake Kutoshiriki Ngono Gizani, Atoa Sababu


Nabii kutoka Nigeria kwa jina Patience Akpabio amewaonya wanawake wenzake kutoshiriki ngono gizani.

Nabii huyu ambaye ni mwandishi wa vitabu vya injili aliandika haya katika mtandao wa Facebook ambapo aliamua kutoa hisia zake kuhusu kufanya tendo la ndoa gizani.

 Ikumbukwe ya kwamba, tangia enzi za kale, wanandoa wengi hupendelea sana kushiriki ngono gizani, kumaanisha ni nadra sana washiriki ngono mchana.

Nabii Patience Akpabio alisisitizia wanandoa kuhakikisha kuwa vyumba vyao vina mwangaza wa kutosha wakati wa ngono ili kuhakikisha kuna mihemko mizuri na uwazi.

Aliandika;

“Huu ni mwaka 2020 hakuna kufanya mapenzi gizani, ukiwa na mume wako wacha taa ziwake, watoto wanaozalishwa wakati mnafanya tendo huku mkiwa gizani, wanakuwa na maono tofauti ya kidunia kuliko wale waliozaliwa kipindi kuna mwanga wa taa” 

Anaamini kuwa kushiriki ngono gizani hufanya kalamu (uume) hufanya kazi kama kipofu lakini kwa mwanga huweza kuelekeza kalamu kwenye kitabu cha mwanamke bila shida yoyote.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad