Nadharia ya Miaka 1,000 Duniani ni Sawa na Siku Moja Mbinguni si Sahihi Kabisa
0
May 30, 2020
Salute..
kuna msemo sijui tulifundishwa au tulisoma wenyewe kwenye vitabu vyetu vya dini (Bibble & Qu'ran) msemo huo unasema kua Miaka elfu moja duniani ni sawa na siku moja mbingu, kiukweli kwa uelewa wangu mdogo wa maswala ya Theologia na Physics nasema huu msemo ni uongo ina wezekana waliotufundisha au tulipousoma kwenye vitabu tuliutafsiri tofauti.
.......
Ref kutoka Qu'ran: Surat Hajj 47, allah anasema kuwa siku moja ya Allah ni sawa na miaka elfu moja "1,000".
Ref from Bible: Zaburi 90:4 Kwako miaka elfu moja ni kama siku moja tu, ni kama jana ambayo imekwisha kupita, kwako ni kama mkesha mmoja wa usiku
2Petro 3:8 Lakini, wapenzi, msilisahau neno hili, kwamba kwa Bwana siku moja ni kama miaka elfu, na miaka elfu ni kama siku moja
Haya ndio maandiko ambayo yamefanya kuenea kwa msemo ambao mimi kwa muono wangu naona si kweli kwa jinsi watu wanavyo
yatafsiri, mimii naelewa hivi kuhusu haya maandiko and I hope theseare aint Blasphemy kwani the Almighty hapendi wasiotaka kuhoji...Let's go!
Kwanza kabisa Kiasili Mungu ana sifa kuu ambazo ni Omniscience (Ajuaye yote), Omnipotence (Mwenye uweza na nguvu zote) na Omnipresence (aliyoko kila mahalii).
tunaposema kua kwa Mungu/Mbinguni siku moja sawa na miaka 1000 ya duniani msemo huu unauvunja vipande vipande ile sifa ya Mungu ya kua Ana uwezo wa kila kitu na Hana mwanzo wala mwisho.... Kivipi???????????
duniani sababu kuu ambayo inatufanya twafariki ni kwasababu i)Dhambi ya asili (ii)ili kuweza kubalnce nature na kuruhusu existence ya viumbe vingine duniani (iii)time. Yes tunakufa kwakua kuna muda duniani ambao unatuhesabia siku zetu tunazoishi hapa dunia ..Time is the biggest threat to mankind ndio maana nilisema kwenye mada yangu ya time Travelling kua tukiweza kudhibiti muda basi tunaweza kudhibiti KIFO. Kwa mantiki hiyo nachelea kusema kwamba kama kwa Mungu kuna Muda basi Mungu ana mwanzoo, Mbinguni kuna vifo there is no eternal life at all, Yawezekana basi hakuna Mungu mmoja maana watakua wanapita/wanafariki (God Forgive I feel like I'm going too far).
Kwa mujibu Fundamental physical quantity, the SI-Unit of Time is Second and other si-unit are year, day, month, decade, millisecond, century etc...Hivyo basi kama mbinguni Muda basi Mungu atakua ana muda maalumu aliotokea(ana mwanzo) maana ili muda uweze kuhesabiwa lazima kuwe na jua linalo zunguka, haingii akilini kwamba kila ikifika miaka elfu ya duniani basi Mungu hua analala kwakua jua limezama usiku umeingia haiwezekani.
Ninavyofahamu Mimi kwa Mungu hakuna muda (Timeless) hakuna future wala past kila muda kwake ni present, Mungu hawezi eti kesho nitafanya hivi na hivi big Nope ndio maana malaika hawazeeki wala hawafi maana hakuna Muda waliowekewa unaohesabu miaka yaoo labda technically aliyewaumba anajua umri wao. Sie wanadamu tumewekewa muda ili tuweze kupanga malengo yetu, ili tuweze kuishi umri fulani tulipangiwa na Muumba,,ili siku moja tufe that's all..
Kwa hiyo basi kwa kusema hivo yawezekana msemo huu inawezekana kutokana na ambiguity ya kiswahili chetu wakati unatafsriwa kutaka version ya lugha zingine sie tuliuelewa vibaya. au kwa vyovyote vile ulipokelewa kimakosa kama vitabu vinne vya wakorintho ilivyokua..
Mwisho kabisa niseme kua huu ni muono wangu na sio pie kwamba kila mtu alzima aelewe hivyo..Lakini naamini kwa Mungu ni Timeless
Anybody Concur with me......???????????
~Da'Vinci
JF
Tags