Ndugu Wanne Wafariki Kwenye Tope Wakimwokoa Mwenzao



Watu wanne wa familia moja wamefariki dunia Bagamoyo, walipokuwa wakivua samaki kwenye dimbwi jirani na mto na kuzama kwenye tope.

Kamanda wa polisi mkoani Pwani, Wankyo Nyigesa amethibitisha tukio hilo mjini Kibaha alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

Amesema kuwa tukio hilo lilitokea Mei 14 mwaka huu kwenye kitongoji cha Amani, kata ya Kerege wilayani Bagamoyo wakati ndugu hao walipokuwa wakivua samaki kwenye dimbwi la maji lililopo mto Mkuza.

“Wakati wanavua kwa bahati mbaya mmoja alizama majini na katika jitihada za kumwokoa ndugu yao wengine nao waliingia majini kisha kunasa kwenye tope na kushindwa kujiokoa na kusababisha vifo hivyo” amebainisha kamanda Nyigesa.

Dkt. Ndugulile aeleza alivyoupokea uamuzi wa Rais Magufuli, amuahidi Dkt. Mollel
Amewataja waliofariki kuwa ni Juma Matonange (21), Emmanuel Matonange (21), Felister Matonange (18) na Ashura.

Ametoa rai kwa wananchi kuwa makini na madimbwi na maji kwani kutokana na mvua nyingi ni hatari kama kama ilivyotokea kwa ndugu hao.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad