‘Nilileta Wanaume Karibu 10 Kwetu Wakakataliwa na Wazazi.....

‘Nilileta Wanaume Karibu 10 Kwetu Wakakataliwa na Wazazi.....

Isabel yupo katika njia panda kuhusu maisha ambayo wazazi wake na kaka zake wanataka aishi kwa sababu shinikizo wanazompa kwamba anafaa kuolewa sasa linamkera.

Anasema masaibu yake yalianza miaka mitano iliyopita kwa sababu ya jamaa zake kuingilia maisha yake na kutaka kumchagulia hata mtu atakayemuoa. Anajutia kwamba hajakuwa na ujasiri wa kuweza kuwapuuza na kuendelea na maisha yake akitegemea maamuzi yake mwenyewe. Amekuwa akikutana na wanaume wanaotaka kumchumbi lakini unapofika wakati wa kuwatambulisha kwa wazazi wake, wanaanza kutoa vijisababu vya kumkataa na hatimaye kumfanya aachane nao.


Hata hivyo, baada ya  kusherehekea siku yake ya kuzaliwa alipodikisha umri wa miaka  ya 36 maajuzi, Isabel amegundua kwamba karibu wasichana wote wa rika lake katika kijiji chao wapo katika ndoa au mahusiano ya  kudumu ila yeye yungali nyumbani baada ya kumaliza masomo na kupata kazi  nzuri bila kuwa na mtu wa kumleta nyumbani kama mchumba kumtambulisha. Sasa mama na babake ambao walikuwa wakiwakataa wapenzi wake wa hapo awali ndio walio katika mstari wa mbele kumpa presha kwamba muda wake wa kuolewa umefika .

Mtalaam wa masuala ya uhusiano Charles Wachira anasema sio jambo geni kwa wazazi kutaka kuchukua udhibiti wa maisha ya wanao hata wanapokuwa wakubwa lakini kila mtu anafaa kuwa na busara ya kugundua wakati ambapo mzazi  anapokupotosha kuhusu maisha yako  katika uhusiano au ndoa .


‘Inakuwa vigumu kuwa na uhusiano wa kudumu na kufaa iwapo wazazi wako hawajakuamini kuweza kujifanyia uamuzi wako mwenyewe’ anasema   Wachira .

Anasema, wazazi  hasa akina mama huwa na hofu ya kuwachiliwa watoto wao wanapokuwa wakubwa  kwa sababu ya mapenzi yao kwao lakini hilo halifai kuvuka mipaka hadi kiasi cha kuathiri maamuzi yao wakiwa watu wazima. Kuna visa vya watu kujinyonga kwa sababu ya wazazi kukataa kuidhinisha uhusiano wao na wapenzi waliowaleta kwa sababu ya ubaguzi  kwa misingi ya kipuzi kama vile kabila au dini. Kuhusu suala la  Isabel, Wachira anasema anachofaa kufanya ni kuhakikisha kwamba mtu anayeanza uhusiano naye ni anayemfaa wala sio anayekubalika na wazazi wake .


‘ Iwapo huna mpango wa kuishi  milele na wazazi wako, unafaa kutafuta uhuru katika fikra zako  kujifanyia maamuzi kuhusu maisha yako binafsi. Wazazi wanaweza tu kukupa ushauri wao bali sio kukufanyia uamuzi’ amesema Wachira
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad