Aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu, asimulia jinsi gari lenye alama ya kampuni ya simu ya mkononi tigo lilivyotekelezwa kwenye geti la nyumba yake.
Nyalandu amesema baada ya gari hilo kutekekezwa majira ya asubuhi wahusika waliondoka.
“Gari yenye usajili wa @tigo-GT#T562 DRS lilipakiwa ndani ya Entrance gate ya nyumbani kwangu na wahusika wakaliacha na kuondoka mapema asubuhi ya leo,” aliandika Nyalandu katika ukurasa wake wa Twitter.
“@tanpol kupitia OCD wa Arusha wanakuja kuchunguza mkasa huu na majirani wamejitolea kutoa ulinzi wakati tunajua kilichojiri,”
Alert: Gari yeny usajili wa @Tigo_GT #T562 DRS lilipakiwa ndani ya entrance gate ya nyumbani kwangu na wahusika wakaliacha na kuondoka mapema asbh ya leo. @tanpol kupitia OCD wa Arusha wanakuja kuchunguza mkasa huu na majirani wamejitolea kutoa ulinzi wakati tunajua kilichojiri pic.twitter.com/Ydls5L6Ixj— Lazaro Nyalandu (@LazaroNyalandu) May 30, 2020