PAUL Makonda: Tusherehekee kwa Kupeana Habari Nzuri sio za Kutishana, Wenye Magari Wekeni Mziki Zungukeni mji wote



Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema leo katika kusherehekea sikukuu ya Eid El Fitri jambo la msingi ni kupeana taarifa njema na wenye magari wawashe mziki huku wakishusha vioo na kuzunguka mji wote na sio kupigiana simu zenye kutishana.

“Kila mmoja kwenye familia yake tukunbushane habari njema, baada ya maombi ya shukrani katika hayo mambo matatu tukumbushane kwa kumshukuru Mungu na hatua ya pili tupige story ya mambo mazuri yaliyotokea kwenye familia, semezaneni habari njema msiambizane habari mbaya vitisho hofu mpate nafasi ya kukumbushana story nzuri,” amesema Makomda.

“Story yoyote ambayo nzuri ipo kwenye familia kama mna bibi, babu, mjomba yoyote yule mjadiliane na kupiga story nzuri muwe na furaha ya kutosha,” alisema Makonda.

Makonda amesema jambo la tatu ambalo anawaomba ni kwamba furaha ambayo mtu anakuwa nayo katika familia aisambaze na kwa watu wengine.

“Ukimpigia simu mtu basi muambie habari njema unayempenda muambie habari njema tusipigiane simu za kutishana tusitumiane clip za ovyo leo ni siku ya kupeana taarifa njema,”

Aliongezea kuwa “Hata kama hujawahi kupata mchumba basi leo mtu akupigie simu akuambie bwana kuna mtu antaka kuja kukuchumbia tunataka habari njema,”

Makonda amsema jambo la mwisho katika sherehe ya leo ya kihistoria amewataka watu kupika vyakula vizuri, wenye uwezo wa kuchinja mbuzi wachome, mwenye uwezo wa kuchoma kukua achome na kufanya kile ambacho kinaweza kukupa furaha ndani ya familia yako.

“Ikiwezekana washa gari lako shusha vioo piga mziki zunguka mji wote ukiweza kwenda kuogelea nenda, madijee pigeni mziki mzuri fungueni kama ni baa kama ni familia beba mtoto wako, mkeo mpeleke dinner sehemu nzuri fanya jambo lolote lile ambao lina furaha,” amesema Makonda

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad