Paul Makonda: Wananchi Walioikimbia Dar warudi, Mauti Hauikimbii. Siku ya Jumapili, kila Mtu Afanye Fujo Awezavyo na Kupiga kelele na Vigeregere!


Akiwa katika ujenzi wa daraja la Tanzanite, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amewataka wakazi wake kufanya fujo za hali ya juu ikiwepo kupiga kelele kwa nguvu zote na watu kwenda beach kama ishara ya kumpongeza Rais kwa kuishinda COVID 19.

"Rais Magufuli ametupa siku tatu za kumshukuru Mungu wetu, naamini kila mmoja atafanya ibada ya Shukrani lakini mimi nimeomba Jumapili kila Mtu apige shangwe na vigelegele ikiwa ni ishara ya Shukrani kwa Mungu wetu kwa Makuu aliyotutendea.

Mtakumbuka historia ya Wana wa Israel walichofanya kwenye ukuta wa Yerico, kwaiyo kama wewe una mziki wako nyumbani piga kelele uwezavyo na Tarehe 25 tunaendelea kuchapa kazi kama kawaida" Alisema RC Makonda
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad