Peter Lijualikali Aendelea Kuikalia Kooni Chadema Afunguka Mengine Mazito


MBUNGE wa Jimbo la Kilombero kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) Peter Lijualikali amezidi kuanika namna ambavyo wabunge wa Chama hicho ambavyo wamekuwa wakikatwa fedha zao na kisha kuzuliwa kuhoji matumizi ya fedha na namna zinavyotumika huku akieleza hatishwi na kauli za kwamba Chama kimemtoa mbali kwani hata yeye amekitoa mbali tu.

Siku za karibuni mbunge huyoa ameingia kwenye malumbano na Chama chake baada ya kuamua kubaki na msimamo wake wa kushiriki vikao vya Bunge wakati Chadema ilipotoa maelekezo kwa wabunge wake kutoingia Bungeni ili wakae siku 14 za Lockdown kwa ajili ya kujikinga na Corona.

Akizugumza na waandishi wa habari Mbunge Lijualikali amesema baada ya kuelezea namna ambavyo wabunge wanakatwa fedha, kuna baadhi ya wabunge wa Chadema na Chama hicho wanadai kwamba wanatoa malalamiko kwenye kukatwa mishahara yao wanapotosha."Sakata la wabunge kukatwa au kuchangia Chama , sisi hatukatai wala hatupingi , unapaswa kuchangia Chama na hatupingi kabisa.

"Katika Katiba ni kweli inaelezea wabunge kuchangia chama.Sawa Katiba inasema kila mbunge anachangia kwa ujenzi wa chama ni kweli na nakubali ndio maana nilikuwa natoa, lakini huchangii kitu ambacho hakina matokeO, bali unachangia kwa kujua nini ambacho kinakwenda kufanyika , ndo maana hata wananchi wanapolipa kodi wanajua kodi yao inakwenda kununua dawa, kujenga shule , hospitali, hivyo unapochangia lazima ujue , sio unatoa tu fedha zako halafu huna haki ya kujua zimetumikaje au hata kuhoji namna ambavyo zimetumika.

"Hakuna utawala wa sheria na hakuna demokrasia hapo, kwa hiyo sisi tunakubali tulikuwa tunawajibu wa kulipa fedha kwenye Chama asilimia 20, hata hivyo lazima tujue fedha hizi zinafanya kazi gani? Ndio tunahoji hapa, wengine wanasema mbona CAG hajaona, CAG haingii kwenye vikao vya Chama na wala kujua tuliambiwa nini,"amesema Lijualikali.

Amefafanua kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) yeye anachoangalia ni kile kilichomo kwenye makaratasi , na sisi tunazungumza tulichokubaliana kwenye vikao , kama CAG anakuaga anauliza, hakuja kwenye vikao vya wabunge wakati Mwenyekiti anatujaza.
"Halafu watu wengi hawajui , hivi ni wanachadema wangapi wanajua akaunti mama zote za chama kuwa Mwamba(Mbowe) ndio anayetia saini ikiwemo akaunti ya fedha za ruzuku".

Ameongeza kuwa akaunti za Chama hicho ambao wanatia saini katia akaunti za Chama ni Mwenyekiti wao Freeman Mbowe, Katibu Mkuu wa Chama, Mkurugenzi wa Fedha na mtu mwingine mwingine kutoka Bodi ya wadhamini.

"Mwamba ni Mwenyekiti wa Chama ndio anakaa pale juu , Mwamba huyu huyu ndio anayeteua Katibu Mkuu wake ambaye naye ni mtia saini katika akaunti halafu Mwamba huyu kwa kukaa na Katibu Mkuu ndio wanakaa kushauriana kuteua Mkurugenzi wa Fedha ambaye pia ni mtia saini, na Mwamba mwenyewe naye anatia saini, hesababu za kazi hizi .
Na hesabu iko hivi Mwenyekiti(Mwamba)Katibu Mkuu na Mkurugenzi wa fedha ndio pea yao hiyo.Wawili wanaweza kusaini kusaini kuchukua mzigo(fedha).Hivi mimi ni diwani pale tuna akaunti ya Kata yetu, utaratibu hauruhusu kabisa Diwani kuwa mtia saini, utaratibu huo haupo.

"Hakua Waziri ambaye ni mtia saini wa akaunti za Wizara , hakuna hata akaunti moja ambayo Rais Dk.John Magufuli na hata marai waliopita wanatia saini.Lakini huku kwetu huku Mwamba ndio mtia saini na ndio maana watu wanasema ni SACCOS, kwa hiyo sehemu zote zinazopigwa za hela jamaa ndio anasaini na wenzake halafu mzigo unatoka, kwa hiyo sisi , yaani mimi Lijualikali ambaye nilikuwa jela ninachangia hela kwenye Chama hichi , nilifungwa jela miezi sita na nimekaa ndani miezi mitatu kila mwezi nilikuwa nachangia , watu wa Mwamba hawakuwahi kutoa hata shilingi 100 mpaka leo, yaani Peter Msigwa na timu yake, na kama wanabisha tumuombe Spika atoe vielelezo kama ataona inafaa,"amesisitiza Mbunge huyo na kusisitiza iwapo kanuni zinaruhsu.

Amesema kuwa yeye alikuwa jela lakini anachangia chama hicho lakini Msigwa na watu wake mpaka leo hawajatoa hata shilingi 100 halafu unataka abaki huko(Chadema)."Yaani yaani nikae huku kha! ebu muwe na huruma jamani , ooo tumekutoa mbali, haukuwa hivi, hivi niulize Chama ni nini?Chama ni watu yaani wakati Chadema kinanitoa mbali na sasa hivi kiko wapi? Wakati Chadema inatoa mbali na chenyewe kilikuwa wapi, yaani mimi nilikuwa mbali na chenyewe kilikuwa mbali.

"Kwa hiyo tumepelekana wote , lakini kama Chadema hakikuwa na watu kikatoa nao mbali, ila tumetoka nacho mbali wote , kwa haya ni maneno tu chama kimekutoa mbali , ulikuwa umepauka, chama chenyewe bila watu kinatoka wapi?Ni maneno tu ya kuudhiana , ni maneno ya kawaida tu na uelewa wao mdogo, sasa ukisema maneno haya ndio Ester Bullaya anakwambia bwana usiseme sana kuna kesho, weka akiba ya maneno, kwasababu kuna vitu kama hivi ,"amesema Lijualikali.

MBUNGE wa Jimbo la Kilombero kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Peter Lijualikali akifafanua jambo Mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani) jana jijini Dar,akieleza mambo mbalimbali yanayomfanya akihame chama hicho,ambacho amedai kwa sasa kimepoteza mwelekeo.

Mbunge wa CHADEMA Mhe.Peter Lijualikali akionesha baadhi ya nyaraka mbalimbali za tuhuma dhidi ya chama hicho,alipokuwa akizunga na Waandishi wa Habari jana jijini Dar

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad