Baada ya kuiteka dunia na kugusa vichwa vingi vya habari kwa rekodi za kutazamwa mara nyingi zaidi mtandaoni kwa muda mfupi, video ya Tekashi 69 "GOOBA" imeondoshwa kwenye mtandao wa YouTube.
Video hiyo iliyokuwa inafanya vizuri, kwa sasa haipatikani kwenye mtandao huo kwa madai ya kukiuka masuala ya hatimiliki (Copyright) ambapo ujumbe uliokuja unaeleza kwamba kuna malalamiko yamewasilishwa na mtayarishaji wa Kenya Magix Enga.
Kupitia Instagram akaunti yake, Magix Enga amejinasibu kumuadabisha Tekashi 69 kwa kosa la ku-sample mdundo wake, ameandika "Don't sample my Beats, biggest song delete by Magix Enga." ameandika mtayarishaji huyo wa Kenya.
Magix Enga ameendelea kuwaadabisha wasanii ambao anadai kuwa wanatumia kazi zake kimakosa, alianza kuziteka headlines kwa kuishusha "UNO" ya Harmonize mapema mwaka huu, na sasa yupo kwenye headlines za dunia.
UPDATE: Video ya "GOOBA" tayari imerudishwa YouTube muda mfupi uliopita kwenye chaneli ya (Tekashi 6ix9ine) na ina jumla ya VIEWS 270M+ ikiwa ni wiki 3 tangu ipandishwe.