Rais Kenyatta: Muda Utafika Itabidi Kenya Ifunguliwe....Hatuwezi Kuendelea Kuwaambia Wananchi Wakae Ndani Milele
0
May 23, 2020
Rais Uhuru Kenyatta ametangaza mipango ya kusaidia biashara na raia kusonga mbele katika kipindi hiki cha mdororo wa kiuchumi kwasababu ya janga la virusi vya corona
Kenyatta amehutubia taifa kutoka Ikulu ya rais, Nairobi na kusema kwamba mipango hiyo itagharimu shilingi bilioni 53.7.
Katika hotuba yake, Kenyatta alisema pesa hizo zitagawanywa katika sekta muhimu kama vile miundo mbinu, elimu, biashara ndogo ndogo na za wastani, afya, kilimo, utalii, mazingira na viwanda vya uzalishaji.
Amesema kuwa taifa hilo haliwezi kuendelea kuchukua hatua za kusalia ndani milele.
Amewaambia Maafisa wa Wizara ya Afya kuwataarifu Wakenya kuwa nchi haiwezi kuendelea kufungwa .Amesema hawawezi kuendelea kuwaambia wananchi wakae ndani na ili uchumi uimarike, ni lazima kila mtu awajibike
''Sisi kama serikali, kama serikali zingine, mataifa yote dunia yameanza kuona, hatuwezi kuendelea kusema wakenya tukae nyumbani, hatuwezi kuendelea kusema tu wakenya msiende kufanya biashara, msiende kazini."- Amesema
Uhuru amesema hayo wakati ambapo pia alitangaza kuwa Kenya maambukizi 31 ya virusi vya corona na kufikisha idadi hiyo hadi 1192.
"Hadi kufikia sasa tumepima watu 57,640 ambapo 1192 wamethibitishwa kuambukizwa na wengine karibia 50 wakipoteza maisha yao kwasababu ya ugonjwa huu,'' Amesema
Tags