Serikali Imesema idadi ya Wanaoumwa Corona Katika vituo vya Afya Imepungua


Serikali imesema watu ambao wamepata maambukizi ya ugonjwa wa virusi vya Corona na waliolazwa kwenye baadhi ya vituo maalum vya matibabu imepungua na wengi wao wanaendelea vizuri kiafya.

Hayo yalielezwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Prof Mabula Mchembe wakati alipokuwa anapokea vifaa kinga vyenye thamani ya Sh milioni 700.75 vilivyotokewa na serikali ya China.

Alivitaja baadhi ya vituo vya matibabu ya ugonjwa wa Corona na idadi ya wagonjwa kwa siku ya leo kwa Dar es Salaam na Pwani kuwa hospitali Amana ina wagonjwa 12, kisoka- Mloganzila 6 na kituo cha Kibaha 24.

Prof. Mchembe amewaasa watoa huduma za afya kuwahudumia wote wanaofika katika kituo cha afya bila ubaguzi.

Amesema wapo wagonjwa wengine hawaumwi Corona bali wana magonjwa mengine ambayo yanahitaji huduma za matibabu ya kila siku.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad