Serikali ya China Yasema Kuna Watu Wanaifitinisha na Afrika Katika Mapambano ya Corona


Corona
Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi amesema China itasimama na Afrika mwanzo mwisho katika kupambana na janga la ugonjwa wa virusi vya Corona ambao ulianzia katika jimbo la Wuhan nchini China na baadaye kusambaa duniani kote.

Waziri huyo ametoa kauli hyo wakati akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia Gedu Andargachew ambapo amemhakikisha kuwa China haitaiacha Afrika mpaka kutokomeza ugonjwa huo.

“Wapo wanaotaka kutugombanisha wakiwemo USA, hawatoweza, Afrika ni Ndugu zetu na sera za china kwa bara la afika hazibadilika na wala hazitakuja kubadilika, Wakati huu wa mapambano ni muhimu kuwa na umoja kati yetu na bara hili”

Aidha inaelezwa kuwa idadi ya visa vya wagonjwa katika bara hili lenye watu Zaidi ya bilioni 1 ni Zaidi ya 66,00 na waliopoteza maisha ni Zaidi ya 2,300.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad