Serikali Yaachilia Huru Wafungwa 7,000 baada ya Wawili Kupatikana na Corona
0
May 11, 2020
Wafungwa hao 7,000 waliachiliwa huru baada ya wawili kupatikana na virusi vya Corona. Picha: Hisani.
Serikali Kenya imewaachilia huru wafungwa 7,000 baada ya wawili kati yao kuthibitishwa kuambukizwa virusi vya corona.
Wawili hao waliripotiwa kuambukizwa virusi hivyo katika jela ya Industrial Area. Takriban wafungwa wengine 42 walithibitishwa kutangamana na wawili hao walioambukizwa corona walitiwa karantini ili kuzuia maambukizi zaidi.
Waziri wa usalama Fred Matiangi ameeleza kuwa serikali imelazimika kuchukua hatua ya kuwaachilia huru wafungwa hao ili kuzui uwezekano wa kuvisambaza kwa wenzao.
Gov't frees over 7,000 inmates after 2 test positive for COVID-19
Rashid Aman. picha: MoH
Hatua hiyo imechukuliwa siku mbili tu baada ya waziri mwandamizi katika wizara ya afya Rashid Aman kuahii kuhusu kufanyika vipimo vya virusi hivyo kwenye jela zote nchini.
‘ Naamini kuwa sekta ya huduma za dharura wamepashwa habari kuhusu visa viwili vya maambukizi vilivyothibitishwa katika jela ya Industial Area. Vituo vya kurekebisha tabia ndivyo viko katika hatari kubwa kuhusiana na maambukizi ya virusi vya corona kutokana na hali ya kutangamana humo.’’ Alisema Aman.
Idadi ya waliambukizwa virusi vya corona hadi sasa imefika 700 baada ya watu wengine 28 kuthibitishwa kupatikana na virusi hivyo na wengine takriban 32 kufariki kutokana na virusi hivyo.
Tags