TAKUKURU Yaanza Kuichunguza CHADEMA Juu Ya Tuhuma Za Matumizi Mabaya Ya Fedha.



Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru), imeanza kuchunguza tuhuma za matumizi mabaya ya fedha, inazokikabili Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). 
 
Hivi karibuni, kumekuwepo na madai yanayotolewa na baadhi ya wabunge juu ya matumizi mabaya ya fedha walizochanga kila mwezi kwa mujibu wa Katiba.

Baadhi ya waliotoa shutuma hizo ni; wabunge wa viti maalum; Susan Maselle, Joyce Sokombi na Peter Lijualikali wa Kilombero ambao wote wametangaza kukihama chama hicho.

Kwa nyakati tofauti, wabunge hao, Maselle na Sokombi walisema mara baada ya Bunge kuvunjwa watahamia NCCR-Mageuzi huku wakisema, hawana shida na kuchangia fedha hizo lakini matumizi yake hayaeleweki.

Leo Jumatano, tarehe 27 Mei 2020, Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru  Brigedia Jenerali John Mbungo amesema wameanza kuwahoji baadhi ya watu. 

 “Kwa mujibu wa taarifa tulizo nazo, kuna matumizi mabaya ya fedha za michango ya wanachama, ambayo kwa mujibu wa katiba yao wanadai imeanishwa wachangie.”

“Lakini, matumizi yake ndio wanatilia mashaka, kuna fedha nyingi zinatumika ndivyo sivyo, kwa mujibu wa makubaliano yao,” amesema Jenerali Mbungo.

“Kwa hiyo, tunachunguza matumizi yasiyo sahihi ya fedha zao, Takukuru inayomamlaka ya kuchunguza taasisi yoyote iwe ya umma, watu binafsi, chama, klabu, iwe chochote Takukuru wanaingia kufanya uchunguzi, ilimradi kuwe na ubadhirifu au matumizi mabaya ya fedha na rushwa,” amesema bosi huyo wa Takukuru.

Amesema, wameanza kuwahoji wanachama waandamizi  na viongozi wa Chadema, wabunge waliotoa tuhuma hizo, pamoja na maafisa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Mbungo amewataja baadhi ya watakaohojiwa ni; Dk. Vincent Mashinji, aliyekuwa Katibu Mkuu Chadema, ambaye kwa sasa amehamia Chama cha Mapinduzi (CCM), John Mrema, Mkurugenzi wa Itifaki na Mambo ya Nje Chadema, pamoja na mhasibu mkuu wa chama hicho, Dk. Roderick Lutembeka.

Aidha, Jenerali Mbungo amesema wameshindwa kumhoji Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema Taifa, kuhusu sakata hilo, kwa kuwa aliieleza TAKUKURU kwamba yuko nje ya jiji la Dar es Salaam.

Amesema, taasisi hiyo imeshaanza kukusanya nyaraka mbalimbali, zinazohusiana na tuhuma hizo. 

Credit: Mwanahalisi

Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mbungo, Tuna Imani na Utendaji wako na Timu yako kwa Ujumla wake. Na kuweza kufikia mpaka ugawaji wa pesa kwa maandalizi ya uvunjaji Amani na wasambazaji wake kwa vijana wa Bajji na BodaBoda kabla ya Machinga.

    Hawa ikithibitika ni lazima Biswalo achukue hatua stahiki, viashiria vipo na Dalili tosha.

    Amanii na Usalaamawa Taifa letu, Hatuwezi kuuwa katika Mikono ya waharibifu wachache huku tukiwaachia waendelee kujilimbikizia kwa Nia Ovu
    na Malengo ya Uharibifu na kuvunja Utulivu na Amani yetu chanzo ni pesa
    za Kodi zetu Walala Hoi.

    Mungu ibariki Tanzania.
    Mungu Dumisha Amani na Usalama wa Tanzania.

    Vibaraka na Mamluki Mungu Awashinde.!!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Swadakta!! Hawa na Saccos yao
      wamekaa Kiuvunjifu vunjifu na
      Ajenda zao mafichoni. Wata Umbuka kwa Mbongo..!! hakuna Mjadala hapo.Kidume yuko kazini.

      Delete
  2. Mbungo, Tuna Imani na Utendaji wako na Timu yako kwa Ujumla wake. Na kuweza kufikia mpaka ugawaji wa pesa kwa maandalizi ya uvunjaji Amani na wasambazaji wake kwa vijana wa Bajaji na BodaBoda kabla ya Machinga.

    Hawa ikithibitika ni lazima Biswalo achukue hatua stahiki, viashiria vipo na Dalili tosha.

    Amani na Usalama wa Taifa letu, Hatuwezi kuuwacha katika Mikono ya waharibifu wachache huku tukiwaachia waendelee kujilimbikizia kwa Nia Ovu na Malengo ya Uharibifu na kuvunja Utulivu na Amani yetu chanzo ni pesa
    za Kodi zetu Walala Hoi. HAIWEZEKANI.

    Mungu ibariki Tanzania.
    Mungu Dumisha Amani na Usalama wa Tanzania.

    Vibaraka na Mamluki Mungu Awashinde.!!
    Na kuwaangamiza kama zilivyo Nia Zenu.

    Magu endelea Kututmikia Mungu akulinde

    ReplyDelete
  3. Ni wengi waliolalamika ikiwepo Naibu mawaziri wa Afya/Tamisemi abao walisha Omba katika Bunge kwa pesa zao Warudishiwe toka Dec 2019.

    Ukweli wa Ubadhirifu uko Dhahiri Shahiri.

    Mbungo tunakuombea mungu kulifanyia

    hili kazi inayo stahiki kwa Masilahi
    mapana ya Taifa letu.

    Vipato vya ujanja ujanja na kupeana
    ulaji na Madili kifamilia Na ukodishaji wa viti vya uwakilishi ni
    ukiukwaji wa Malengo/Sera/Maadili na
    Mrengo wa Kanuni za Uendeshaji kufikia
    Dhumuni Kusudiwa.

    Awamu yetu ya Tano na Sita ni kutupeleka katika Tanzania Mpya ya Uchumi wa Viwanda uchumi wa Kati.

    Mbinu za Wacheleweshaji Zitaumbuka.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad