Unaweza kusema mzigo wa dawa ya kupamana na Corona inayotengenezwa nchini Madagascar punde itaanza kuonekana katika mitaa ya Tanzania baada ya Serikali kuwasili katika nchi hiyo kiuchukua.
Katika ukurasa wa mtandao wa Wizara ya mambo ya nje zimewekwa picha zikimuonyesha waziri wa mambo ya nje ya Tanzania Waziri wa Mambo ya Nje profesa palamagamba Kabudi akiwa nchini Madagascar na ndege ya Serikali na akikabidhiwa dawa hizo.
Hata hivyo pamoja na kukabidhiwa kuna picha inamuonyesha Profesa kabudi akinywa dawa hiyo pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Madagascar Tehindrazanarivelo Djacoba As Oliva.