Tiba ya Dharura ya Corona Yapatikana, Marekani Yantangaza Dawa
0
May 02, 2020
MAMLAKA ya Dawa na Chakula (FDA) nchini Marekani imeidhinisha matumizi ya dharura ya dawa ya Ebola, remdesivir, ianze kutumika kutibu virusi vya corona.
Kufuatia hatua hiyo, dawa hiyo itaanza kutumiwa na watu walioathiriwa zaidi na homa ya mapafu (COVID-19).
Majaribio ya hivi karibuni yameonyesha kuwa dawa ya remdesivir inayozalishwa na kampuni ya dawa ya Gilead ilisaidia kupunguza muda wa mgonjwa kupata ahueni ya COVID-19.
Hata hivyo wataalamu wametahadharisha kuwa dawa hivyo isichukuliwe kama suluhisho la virusi vya corona, na kwamba FDA imeidhinisha matumizi ya dharura pekee.
Taasisi ya kupambana na magonjwa ya kuambukiza nchini Marekani katika utafiti wake wa hivi karibuni ilibaini kuwa remdesivir inaweza kupunguza muda wa dalili kuonekana kwa muathirika kutoka siku 15 hadi siku 11.
Licha ya mafanikio hayo ya awali, bado ni kitendawili kama dawa hiyo inaweza kuzuia vifo vitokanavyo na virusi vya corona.
Tags