Ugonjwa Uliomuondoa Jaji Mkuu Mstaafu Ramadhani Huu Hapa, Leo Kuagwa Kitaifa Karimjee



Jaji Mkuu Mstaafu, Augustino Ramadhani ataagwa leo kitaifa katika viwanja vya vya Karimjee na mazishi yatafanyika kesho Kimara jijini Dar es Salaam.

Kiongozi huyo ataagwa kitaifa kwa mujibu wa sheria ya mazishi ya viongozi wa kitaifa ya mwaka 2006.

Taarifa iliyotolewa na msajili wa Mahakama ya Rufani, Kelvin Mhina jana ilieleza kuwa taratibu za mazishi na maandalizi zinafanywa na kusimamiwa na kamati ya mazishi ya viongozi wa kitaifa  inayoongozwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

‘Siku ya Ijumaa (leo) kutakuwa na mazishi ya kitaifa viwanja vya Karimjee kuanzia saa 6:00 hadi saa 8:00 mchana,” ilieleza taarifa hiyo.



Aidha, Mhina alisema Jaji Ramadhani atazikwa kesho Jumamosi katika eneo la Makaburi ya familia yaliyopo Kimara King’ongo jijini Dar es Salaam.

Mazishi yatafanyika saa tisa alasiri na kutanguliwa na ibada itakayofanyika katika kanisa la Anglikana la Mtakatifu Albano kuanzia saa 6:00 mchana jijini.

Jaji Ramadhani alifariki dunia Aprili 28, 2020 majra ya saa 2:05 asubuhi katika hospitali ya AgaKhan jijini Dar es Salaam baada ya kuugua kwa muda mrefu maradhi ya saratani na mwishoni kupata mshtuko wa moyo (Heart Attack).

Marehemu Jaji Ramadhani alianza kuugua mwaka 2011 na kugundulika kuwa na ugonjwa wa saratani ambao alipatiwa matibabu katika hospitali mbalimbali nje na ndani ya nchi. Hospitali alizotibiwa ni Apolo na Banglow nchini India, Afrika Kusini, Nairobi na Dar es Salaam.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad