Uhispania yakaribisha watalii kutoka pande zote duniani


J


Uhispania sio tu inakaribisha bali inahimiza pia utalii wa kimataifa kuanzia mwezi Julai, Hayo yamezungumzwa na waziri mkuu wa nchi hiyo. 

"Uhispania inatarajia watalii, kuanzia mwezi Julai" Pedro Sanchez amezungumza hayo katika mkutano na waandishi wa habari na kuendelea kwa kusema kuwa "Watalii wa kigeni sasa wanaweza kuanza kupanga likizo zao kwenda Uhispania." 

Uhispania inapata wageni milioni 80 kwa mwaka, na sekta ya utalii inachangia takriban 12% ya Pato la Taifa la nchi hiyo. 

Mlipuko wa corona umeivuruga sekta hiyo kwani wafanyakazi milioni moja katika sekta ya utalii wamesimamishwa kwa muda. 

"Uhispania inahitaji utalii na utalii unahitaji usalama. Tutahakikisha kwamba watalii hawatakuwa hatarini na hawataleta hatari yoyote kwa nchi yetu, "alisema Sanchez. 

Wizara za Uchukuzi na Viwanda zinatarajiwa kutolewa mpango wa kina wiki hii kuhusu itifaki ya afya ambayo itabidi sekta ya utalii ifuate kwani virusi bado vipo. 

"Ninakaribisha taasisi zote za utalii zianze kujiandaa kuanzia leo kuanza tena shughuli," alisema Sanchez. 

Uchunguzi wa Ernst & Young wiki hii uligundua kuwa nusu ya Wahispania hawana matumaini ya kusafiri kwenda likizo wakati huu wote wa msimu wa joto. Asilimia 40 nyingine walisema watatembelea ndani ya nchi huku aslimia 9 tu wanatarajia kusafiri nje ya nchi. 

Swali la kujiuliza kwa sasa ni endapo watalii wa kigeni wanataka kutembelea Uhispania ama la. 

Kufikia sasa, Uhispania imethibitisha karibu kesi 235,000 za COVID-19 na zaidi ya vifo 28,500. 

Baada ya wananchi kufungiwa ndani kwa miezi miwili,maambukizi yameanza kudhibitiwa lakini hayajaisha moja kwa moja. 

Siku ya Ijumaa, nchi hiyo iliripoti maambukizo mapya 446 na vifo 56

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad