Ujerumani Yalenga Kulegeza Mashariti ya Watu Kukaribiana



Ujerumani inapanga kulegeza hatua za watu kukaribiana kuanzia Juni 29, wiki moja kabla ya iliyopangwa hapo awali, na ina lenga kuondoa vizuwizi vya kusafiri kwa mataifa 31 ya Ulaya kuanzia katikati ya mwezi Juni.

Ripoti hiyo inakuja wakati majimbo ya Ujerumani yanajadiliana na kansela Angela Merkel juu ya vipi kulegeza vizuwizi vya watu kuzuiwa majumbani mwao hatua iliyoanza kutumika mwezi Machi kwa nia ya kupunguza kusambaa kwa virusi vya corona.

Mawaziri wakuu wa majimbo 16 ya Ujerumani watajaribu hapo kesho kukubaliana na Merkel kuhusu hatua ya kuchukua, ikileta uwiano kuhusu mahitaji ya kuufufua uchumi wa taifa hilo lenye uchumi mkubwa barani Ulaya, unaokabiliwa na mdororo mkubwa tangu baada ya vita vikuu vya pili vya dunia, pamoja na kulinda afya ya jamii.

Gazeti la Bild la Ujerumani limesema kuwa mikusanyiko katika maeneo ya umma haitazidi watu 10, ama ndugu wa familia mbili. Ujerumani imekuwa na idadi ndogo ya vifo 8,302 licha ya idadi ya juu ya maambukizi.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad