Uwezi Amini....Njaa na Umasikini Wakutupwa Vinaitesa Marekani



Spika wa Bunge la Wawakilishi nchini Marekani amekiri kwamba, baada ya virusi vya Corona kuenea nchini humo, hivi sasa nchi hiyo inakabiliwa na ongezeko kubwa la umasikini na njaa.

Bi Nancy Pelosi amesema hayo na kuongeza kuwa, kwa sasa familia nyingi nchini Marekani hazina kabisa usalama wa chakula.

Spika Pelosi amesema bayana kwamba, kwa sasa Marekani inakabiliwa na changamoto kubwa na changamoto hiyo imedhihiri zaidi baada ya kuibuka virusi vya Corona nchini humo janga ambalo limepelekea raia wengi kupoteza ajira na shughuli zilizokuwazikiwaingizia kipato.

Spika wa Bunge la Wawakilishi nchini Marekani (Kongresi) amesema kuwa, viongozi wa nchi hiyo hawajachukua hatua za maana za kukabiliana na changamoto hiyo.


Spika huyo ambaye anatoka katika chama cha upinzani cha Democtar ameeleza kwamba, humusi ya watoto wa familia moja ya Kimarekani haina usalama wa chakula na hali hii imekuwa mbaya zaidi baada ya kuenea virusi vya Corona.

Wakati huo huo, ripoti mbalimbali zinaonyesha kuwa, licha ya ahadi chungu nzima alizotoa Rais Donald Trump wa Marekani za kupunguza kiwango cha umasikini nchini humo, lakini idadi ya watu wanaotaabika kwa ufakiri na umasikini imeongezeka katika miaka ya hivi karibuni.

Inaelezwa kuwa, akthari ya Wamarekani wamekata tamaa kabisa na utendaji wa sasa na wa baadaye wa serikali ya Trump katika suala zima la uchumi na hivyo wanazieleza siasa za Trump kwamba, ndizo zilizopelekea kuongezeka umasikini nchini humo na hivyo kuyafanya maisha yao kuwa magumu siku baada ya siku.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad