Views za Ayo TV Zapaa Baada ya Kumpost Diamond Platnumz...Ashauriwa Kuacha Kubagua WCB ili Afanikiwe
0
May 05, 2020
Ayo Tv, Millard ayo channel ya youtube zamani ilishazoeleka kuingiza hata video 10 kwa mpigo kwenye orodha ya video zinazovuma (trending videos), Ni kipindi ambacho kijana hakuwa na mpinzani youtube akiweka video yani fasta tu views laki na ushehe tayari, kijana alipiga mpunga acha kabisa,
Ila miaka michache nyuma alipoingia kwenye ugomvi wa wcb na clouds fm, alifanyauamuzi ulioua channel yake kwasababu aliamua kuacha kupost video za wcb, wafatiliaji wa channel yake wakapungua, views za video zake zikawa chache na kupelekea kuanza kupokea pesa kidogo sana, ila wakati huo huo channel changa zilijijenga na kumfunika kabisa millard ayo kwa kupost maudhui ya WCB.
Leo masaa tisa yaliyopita, kaweka video ya Diamond tayari ina views karibia laki, ni kitu ambacho hakijatokea kwa muda mrefu kwenye channel yake, ni kama muujiza, kwa views hizi kwa makadirio ya fasta fasta atakua kaingiza laki 3, na video bado ni mbichi bado inaendelea kusomba views.
alizoea kuingiza zaidi views millioni 50 kwa mwezi kitu lichomfanya apokee zaidi ya milioni 70, alipoanza ukauzu mwezi mzima tia maji tia maji ana views milioni hapo ana milioni 2 tu inaishia yote kulipa wafanyakazi
Kwa ushauri tu naona millard arudi kwenye sifa za kuwa mwandishi wa habari tuliyemzoea ambae alikuwa hana upendeleo wala ubaguzi, aliacha kupost habari za wcb alitegemea nini????
Angalia Hapa chini Ushahidi wa Viewers wa Video Alizoweka Jana, ya Diamond ina Viewes 97,000 , nyingine sasa....
By Dudu Jeupe/JF
Tags