Vifo vya COVID-19 vyapindukia 300,000
0
May 15, 2020
Idadi ya vifo vilivyotokana na maambukizi ya virusi vya corona duniani kote imepindukia watu 300,000, ambapo vingi vya vifo hivyo vimetokea Ulaya na Marekani, tangu kuzuka kwake huko China, mwishoni mwa mwaka uliopita
Brazil imesajiri maambukizi mapya ya virusi vya corona 13,944 na vifo 844. Rekodi hizo zimetolewa na wizara ya afya zinawakilisha katika kipindi cha masaa 24. Idadi jumla tangu kuanza kwa mripuko huo ni maambukizi 202,918 na vifo 13,933. Katika eneo hilo hilo la Amerika ya Kusini Imerekodi vifo vipya 257 na maambukizi 2,409.
Kiwango hicho kikitajwa kuwa cha juu zaidi tangu kuingia kwa maambukizi hayo nchini humo. Taarifa hizo mpya zinafanya jumla ya maambukizi kufikia 42,595 na vifo 4,477.
Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa Mei 19 atakutana na Mtendaji Mkuu wa kampuni kubwa ya kutengeneza madawa-Sanofi, Paul Hudson, baada ya siku chache zilizopita mkuu huyo kuigadhibisha serikali, kwa kusema baadhi ya mataifa yatapewa kupaumbele katika upatikanaji wa chanjo ya virusi vya corona. Hudson aliifuta kauli yake hiyo ya awali, mapema Alhamis kwa kusema ni muhimu kwamba chanjo yoyote ya corona, ikifika kwa wote katika pembe tofauti za ulimwengu.
Mkuu wa Shirika la Afya Duniani kwa Ulaya, Hans Kluge amesema kasi ya usambaaji wa virusi vya corona kwa Ulaya, inapungua, lakini ameongeza kuwa lazima mataifa yaendelea kuwa madhubuti katika kukabiliana na janga hilo. Amesema funzo lililopo kwa sasa ni kwamba hakuna muda wa kusherehekea, lakini muda wa kujiandaa.
Kumekuwepo na mfumo madhubuti wa afya lakini unaweza kuzidiwa nguvu katika majuma machache tu. Ulaya bara ambalo limeshambuliwa vikali na virusi, ambapo mataifa kama Italia, Uhispania na Ujerumani ni miongoni mwa mengine 10 ambayo yana idadi kubwa ya maambukizi na vifo. Ujerumani inatarajiwa kuanza kuchukua hatua za kulegeza masharti ya mipakani Jumamosi, wakati mataifa mengine kadhaa ya jirani yatarajaiwa kuichukua hatua kama hizo kuanzia Juni 15. Umoja wa Mataifa umesema janga la corona limesaabisha matatizo ya akili duniani kote.
Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell ameitolewa wito China kuchangia pakubwa katika mambapmbano didi ya janga la corona na kuongeza kwamba, kunapaswa kuwepo na uchunguzi huru wa kubainisha chimbuko la janga hilo la ulimwengu. Katika makala maalumu kwenye gazeti Frankfurter Allgemeine la Ujerumani, mwanadiplomasia huyo amesema China inapaswa kuchukua hatua kuuzuia ulimwengu magonjwa yanayoweza kuzuka katika siku za usoni. Virusi vya corona vilizuka mjini Wuhan China, Desemba na baadhi ya nchi, ikiwemo Marekani na nyingine za Ulaya zimeikosoa kwa namna ilivyoshughulikia mripuko huo. Borell pia amesema China inawajibika katika mambo kadhaa ya ufanikishaji wa tiba na chanjo lakini pia kuyasaidia mataifa yanayoendelea ambayo yameathiriwa na mripuko huo kwa kutoa mikopo nafuu.
Tags