Virusi vya Corona "Obama Asema Uongozi wa Donald Trump Umefeli"



Aliyekuwa rais wa Marekani Barrack Obama kwa mara nyingine tena amemkosoa mrithi wake Donald Trump kwa jinsi anavyolishughulikia suala la virusi vya corona.

Katika hotuba kwa hafla iliyopeperushwa kupitia mtandao, alisema kwamba mlipuko wa virusi vya corona umedhihirisha kwamba maafisa wengine hawafanyi kazi walioajiriwa kusimamia.

Amesema kwamba ni 'janga la machafuko' jinsi Trump anavyoangazia suala hilo , katika mkutano uliovuja wiki iliopita.

Rais huyo wa zamani pia aliwahutubia wanafunzi wa shule ya upili katika sherehe ilioandaliwa na LeBron James na ilikuwa mojawapo ya programu maalum ambayo ilishirikisha watu maarufu kama vile ndugu wa Jonas, Megan Rapinoe, Pharrell Williams na mwanaharakati wa elimu Malala Yousafzai.

Katika hotuba yake kwa takriban zaidi ya taasisi 10 za wanafunzi weusi na vyuo vikuu, bwana Obama alisema kwamba Covid-19 ilifichua mianya na makosa katika uongozi wa taifa hilo.

''Zaidi ya chochote kile janga hili linaonesha wazi kwamba wengi wa maafisa walio uongozini hawajui wanachofanya'', alisema.

Zaidi ya watu 1,200 wamefariki kutokana na virusi vya corona nchini Marekani katika kipindi cha saa 24, kulingana na takwimu mpya kutoka Chuo kikuu cha John Hopkins.

Idadi ya watu waliofariki ni 89,000, ambayo ndio ya juu zaidi duniani.

Bwana Obama pia alizungu jiomzia kwa urefu jinsi virusi hivyo vinavyozidi kuiathiri jamii ya watu weusi nchini humo.

''Ugonjwa kama huu unafichua ukosefu wa usawa uliopo na mzigo wa ziada ambao jamii ya watu weusi wamekuwa wakikabiliana nao katika historia ya taifa hili'', alisema.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad