Vita ni Vita Mura..Kiongozi wa ISIS Nchini Iraq Auawa Katika Shambulizi la Anga


Vita ni Vita Mura..Kiongozi wa ISIS Nchini Iraq Auawa Katika Shambulizi la Anga

Kikosi cha Kupambana na Ugaidi cha Jeshi la Iraq kimetangaza habari ya kuangamizwa kinara wa kundi la kigaidi na ukufurishaji la Daesh (ISIS) nchini humo, Mu'taz al-Jubouri katika shambulizi la anga.

Taarifa iliyotolewa jana Jumanne na kikosi hicho imesema kuwa, kamanda huyo mkuu wa Daesh nchini Iraq, Mu'taz al-Jubouri ambaye pia anafahamika kama Hajji Taysir ameuawa katika shambulizi la anga lililofanywa na muungano wa kimataifa wa kupambana na ugaidi katika mkoa wa Deir al-Zour, mashariki mwa Syria.

Haya yanajiri chini ya wiki moja baada ya Idara ya Intelijensia ya Iraq (INIS) kutangaza habari ya kumtia mbaroni kamanda mwingine wa ngazi za juu wa Daesh, Abdul-Nasser Qardash ambaye hapo awali alitazamiwa kuchukua nafasi ya Abu Bakr al-Baghdadi.

Mapema mwezi huu wa Mei, Kamandi Kuu ya Jeshi la Iraq ilizindua operesheni kali dhidi ya mabaki ya wanachama wa kundi la kigaidi na ukufurishaji la Daesh (ISIS) nchini humo.

Operesheni hiyo ilizinduliwa siku chache baada ya kundi la kigaidi na ukufurishaji la Daesh kuanzisha upya harakati zake katika mikoa kadhaa ya Iraq ikiwemo Salahuddin, Diyala, Babil na al-Anbar kwa msaada wa Marekani.


Mwezi uliopita wa Aprili, chanzo kimoja cha usalama nchini Iraq kilifichua kuwa, kwa mujibu wa taarifa za kiintelejensia zilizopatikana, Abu Ibrahim al-Hashimi al-Qurashi, kiongozi mpya wa kundi la kigaidi na ukufurishaji la Daesh amepenya nchini humo kwa msaada wa askari magaidi wa Marekani.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad