Vurugu mkutano wa Waitara, Meya jiji la Mwanza alazwa rumande




POLISI Mkoa wa Mwanza nchini Tanzania, limemkamata na kumhoji, Meya wa Jiji la Mwanza, James Bwire kwa tuhuma zinazomkabili. 

Bwire ambaye ni Diwani wa Mahina kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), anatuhumiwa kuandaa kikundi cha watu, waliovuruga mkutano wa Naibu Waziri wa Tamisemi, Mwita Waitara alioufanya katika moja ya kata za Jiji hilo tarehe 27 Mei, 2020. 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jumanne Muliro akizungumza na waandishi leo Jumamosi tarehe 30 Mei, 2020 amesema, walimkamata jana jioni Meya Bwire na kumhoji kwa saa 4 kisha wakamalaza rumande. 

“Baada ya kuwa hapatikana kwa urahisi, askari polisi ambao moja ya jukumu lao kumfuata na akaletwa jana jioni kwa mahojiano kulingana na tuhuma nzito ambazo sisi tulizipata.” 

“Ni kweli alishikiriwa na kwamba tarehe 27 Mei 2020, Naibu waziri wa Tamisemi (Mwita) alifanya kikao katika moja ya Kata jiji la Mwanza na zikapatikana taarifa meya wa jiji hili, aliandaa kikundi cha watu ambacho kikao kinafanyika, kilifanya fujo, kikatoa maneno ya kashfa na kejeli dhidi ya waziri na Serikali na kusababisha kuvunjika kwa kikao kile,” amesema 

Amesema, kutokana na tuhuma zito, walimhoji kwa saa nne na kutokana na mazingira, alipumzishwa na kuendelea tena kwa mahojiano hadi alipomaliza leo na kuachiwa kwa dhamana.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad