Wabunge waliofariki dunia Tanzania wafikia tisa


Balozi Mahiga ambaye ni mwanadiplomasia mashuhuri anakuwa mbunge wa tisa wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufariki dunia.

Bunge hilo la 11 linaloongozwa na Spika Job Ndugai lilizinduliwa na Rais John Magufuli Novemba 20 mwaka 2015.

Ratiba iliyotolewa na Ofisi ya Bunge inaonyesha mkutano wa 19 wa Bunge la bajeti ya mwaka 2020/2021 unaoendelea jijini Dodoma utahitimishwa Jumanne ya Juni 30 mwaka 2020 kwa Rais Magufuli kutoa hotuba ya mwisho ya kulifunga.

Wakati uhai wa Bunge ukielekea ukingoni, muhimili huo umejikuta ukipata pigo kwa wabunge wake watatu kufariki dunia katika kipindi cha wiki mbili zilizopita.

Wabunge hao ni; Dk. Getrude Rwakatare wa Viti Maalum (CCM) aliyefariki dunia Aprili 20, 2020. Dk Rwakatare alikuwa Askofu wa Kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni B, Dar es Salaam.

Majonzi yanayotokana na kifo hicho cha Dk. Rwakatare yakiwa hayajatulia, mbunge mwingine wa Sumve (CCM), Richard Ndassa naye akafariki usiku wa kuamkia tarehe 29 Aprili 2020 akiwa jijini Dodoma.

Taarifa za majonzi kwa muhimili zilianza mwaka mmoja tangu kuzinduliwa kwake kwa Mbunge wa Dimani kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Hafidh Ali Tahir kufariki dunia tarehe 11 Novemba 2016.

Tarehe 31 Machi 2017, DK. Elly Macha aliyekuwa mbunge wa viti maalum kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) alifariki dunia.

Miezi takribani nane baadaye, mbunge wa Songea Mjini kupitia CCM, Leonidas Gama alifariki dunia tarehe 24  Novemba 2017. Tarehe 26 Mei 2018, wananchi wa Buyungu walimpoteza mbunge wao Mwalimu Kasuku Bilago wa Chadema.

Julai 2 mwaka 2018, Mbunge wa Korogwe Vijijini  Steven Ngonyani Maarufu Professa Maji Marefu alifariki.

Tarehe 15 Januri 2020, Mbunge wa Newala Vijijini Rashid Ajali Akbar alifariki dunia.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad