Wafuasi wa CHADEMA wakamatwa kwa kufanya fujo katika mkutano wa NCCR Mageuzi



NA Timothy Itembe Mara.

Watu watatu wanaosadikiwa kuwa wamachama wa Chama cha Demokorasia na maendeleo Chadema wamekamatwa na jeshi la Polisi wilayani Tarime kwa makosa ya kuvamia eneo lililokuwa limeandaliwa na Chama cha NCCR Mageuzi kwaajili ya kuongea na vyombo vya habari juzi.

Akiongelea kukamatwa kwa watuhumiwa hao mkuu wa wilaya Tarime,Mtemi Msafiri alisema kuwa watu watatu wanaosadikiwa kuwa wafuasi wa Chama cha Demokorasiaa na maendeleo Chadema wamekamatwa na jeshi la polisi kwa kuwafanyia fujo na kuwaruishia mawe wanachama wa Chama cha NCCR Mageuzi mahali ambao walikuwa wameandaa kuongea na vyombo vya habari juzi.


Msafiri alikema kitendo hicho ambapo alisema kuwa jeshi la polisi linawashikilia wafuasi wa Chadema watatu huku likiwahoji na upelelezi ukikamilika watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani ili kujibu mashitaka ya tuhuma ambayo yanawakabili.


Pia mkuu wa wilaya hiyo aliongeza kusema kuwa wale wote waliohusika katika kitendo cha kufanya fujo wataendelea kusakwa mahali  popote walipo  hadi hapo watakapokamatwa na kufikishwa kwenye mkono wa sheria ili kukabilioana na tuhuma zinazowakabili.

"Nimesikitishwa sana na kitendo cha wafuasi wa Chama cha Demokorasia na maendeleo Chadema kwenda na kuwafanyia fujo huku wakiwarushia mawe wanachama wa Chama cha NCCR Mageuzi kwenye eneo walilokuwa wametenga kuongea na vyombo vya habari kitendo hicho hakikubaliki ni kkinyume cha sheria tutawasaka mahali popote walipo ili tuhakikishe tunawakamata na kuwafikisha sehemu husika wale wote waliohusika"alisema Msafiri.

Mkuu wa wilaya hiyo alimaliza kwa kusema kuwa Tarime sio kisiwa cha matukio yasiyokubalika kisheria bali ni wilaya yenye kuishi kwa kuzingatia sheria za nchi zilizopo na kuwa haiingii akilini watu kuishi kwa kujichukulia sheria mkononi na kama Mtu au chama kimekwazwa kwa namna yeyote kunahaja ya kulalamika sio vinginevyo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad