Wahusika katika mauaji ya binti mdogo wakamatwa Uingereza



Wanaume wengine watatu wameshtakiwa kwa mauaji ya Aya Hachem, msichana wa Kiislamu aliyepigwa risasi na kuuawa mchana kweupe huko Blackburn, Uingereza siku ya Jumapili. 

Polisi wa Lancashire wamesema Uthman Satia, 28, Judy Chapman, 26, na Kashif Manzoor, 24, wameshtakiwa kwa mauaji ya Hachem,binti wa miaka 19. 

Polisi wametangaza mapema Ijumaa kwamba watu wawili wameshtakiwa: Feroz Suleman, 39, na Abubakir Satia, 31. 

Idadi ya watu wanaoshtakiwa sasa imefika watano. 

Watashtakiwa kwa mauaji ya Hachem na vile vile majaribio ya mauaji ya mtu ambaye hakukusudiwa katika shambulizi hilo. 

Polisi wamesema risasi mbili zilifyatuliwa, moja iligonga jengo na nyingine ikampata Hachem. 

Hachem, Mwislamu mwenye asili ya Lebanon na raia wa Uingereza, aliuawa kwa kupigwa risasi wakati alipoenda kununua matunda. 

Wazazi wake walisema katika taarifa kuwa : "Tumeumizwa kabisa na kifo chake na tunapenda kuchukua fursa hii kuwaomba watu ambao wanaweza kuwa na habari yoyote hata kama ndogo ambayo inaweza kusaidia kuwakamata wale waliohusika"

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad