Wanawake Acheni huo Mchezo wa Kujiliza Uongo wakati Hujafikishwa Kileleni


Habari wasomaji wetu nakukaribisha katika darasa letu la mahusiano uweze kujifunza mambo mbalimbali.

Kumekuwa na tabia au hali ya wanawake wengi kupiga kelele au unaweza kusema kutoa sauti wakati wakishiriki tendo la ndoa.

Hali hii imeacha maswali yaani unajiuliza kutoa sauti ni jambo la asili au ni mwanamke mwenyewe anaamua hapa atoe sauti na kwingine asitoe.

Wengine huzani kuwa huyu mwanamke atakuwa alikuwa na nyege sana ama huenda nimemfanya vizuri hayo ni baadhi ya maswali wanajiuliza baadhi ya wanaume.

Mwaka 2011 watafiti wawili mmoja kutoka Chuo Kikuu cha Lancashire na mwingine kutoka Chuo Kikuu cha Leeds wote wa nchini Uingereza walichapisha utafiti wao walioufanya uliokuwa ukihusu utoaji wa sauti wa kati wa kujamiina. Walitaka hasa kujua kwanini wanawake hutoa sauti hizo.

Katika utafiti huo, waliwahoji wanawake 71 wenye umri kati ya miaka 18 na 48 ambao hushiriki mapenzi mara kwa mara juu ya utoaji wa sauti wakati wa kufanya mapenzi.

Katika utafiti huo ulibaini kuwa wanawake wengi huto sauti hizo lakini sio pale tu wanapokuwa wamefika kileleni.

Asilimia 66 walisema kuwa hutoa sauti wakati wa kujamiina ili kuwasaidia wenza wao kufika kileleni haraka, wakati asilimia 87 walisema kuwa hutoa sauti hizo ili kuwaongezea wenza wao kujiamini kwa kile wanachokifanya kuwa wapo sawa.

Wanawake walieleza kuwa mara nyingi hutoa sauti wakati wenza wao wanapofika kileleni. Baadhi pia walieleza kuwa sauti hizo huwasaidia kuwaondolea uoga walionao, hali ya kutojisikia kuwa sawa, wakati mwingine kuondoa maumivu lakini pia kama njia ya kufurahia raha anayokuwa anaipata.

Wataalamu hao walisema kuwa kwa vile wanaume wengi huhusisha utoaji wa sauti na mwanamke kufika kileleni, basi baadhi ya wanawake hutoa sauti hizo kwa uongo ili tu kuwaridhisha wenza wao waone kila kitu kipo sawa.

Imeelezwa kuwa wakati mwingine huwa ni vigumu sana kuelezea kila kinachotokea wakati wa kijamiiana kwa sababu kila mtu huwa na utashi wake.

Lakini kitu wataalamu walichokubaliana ni kuwa sauti hizo zinaweza kumsaidia mwenza kujua kama anachofanya ni sasa hivyo aendelee au aache, aongeze au apunguze.

Pia kuna baadhi ya wanawake hutaka kutoa sauti kutaka kumuibis mwanaume wake ili kumuonyesha amemridhisha wakata hata hajawahi kufikishwa kileleni.

Mwanamke kama huyu hukuta yupo kimaslahi zaidi yaani huwa anataka fedha na sio kufurahia mapenzi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad