Wanawake Acheni Jeuri ya Fedha Katika Mapenzi la Sivyo itakula Kwenu
0
May 31, 2020
Wapo wasichana na wanawake ambao wamekata tamaa za kuolewa kwa sababu mbalimbali ikiwamo kutendwa na wenza wao waliotangulia au kufanyiwa vitendo vya ukatili.
Wanawake au wasichana wa aina hii hawawezi kutofautiana na mitizamo waliyonayo hadi hapo watakapopata elimu ya saikolojia.
Hawa ni wanawake ambao tunajikuta wanaishi wenyewe kwenye nyumba zao na hawana uhusiano kabisa na aina ya wanaume.
Madhara makubwa yanayoweza kuwakuta wanawake au wasichana wa aina hii ni kujikuta wanajiingiza kwenye vilevi vya pombe kali na kuharibu kabisa mfumo wao wa maisha.
Nikiacha wanawake wa aina hii wapo wale ambao wao hawana tukio lolote baya unaloweza kusimuliwa ukasema kweli ameumizwa au amefanyiwa kitendo cha ukatili.
Sanasana utamsikia akisimulia labda mwanaume alimuacha akaona mwanamke mwingine au mwanaume wa kwanza alimuacha kwa sababu hakuwa chaguo lake na sababu ambazo kwa ufupi hazina mashiko ya kumfanya akate tamaa ya maisha.
Wanawake wa aina hii ukichunguza sana utabaini wamejawa na kiburi cha pesa. Kiasi kwamba anataka mwanaume awe chini yake.
Baadhi ya wanawake wakishakuwa na fedha au vyeo makazini kuna namna wanainua mabega na kutotaka kujishusha kwa mwenza wake kwa ufupi wanajisahau.
Anaamini akiwa bosi hawezi kuwa chini au kumnyenyekea mwanaume ambaye ni mpenzi wake au mume wake kabisa.
Mwanamke wa aina hii inafika wakati anaanza kuona kila mwanuame si saizi yake anatamani kuwa yule aliyempita kiwango cha elimu au uwezo zaidi yake.
Akiamini anaweza kumnyenyekea na kumsikiliza tofauti kabisa na ambaye yupo chini yake.
Mitizamo kama hii kwa wanawake na wasichana ambao hawajaolewa inawafanya kuendelea kukosa wanaume sahihi wa kuwaona kwa sababu wanaamini bado hawajapata mtu sahihi kimtizamo.
Ukiwa mwanamke unayejitambua na una mpango wa kuwa mke wa mtu au mama mtarajiwa unapaswa kujishusha na kuwa na heshima kwa mpenzi wako kama kweli unania ya dhani ya kuwa naye.
Wanawake muachane na dhana potofu kuwa na mwauame uliyemzidi kipato au kiwango cha elimu si saizi yako ilihali unaona anakufaa kabisa kwenye maisha yako.
Tabia kama hizi kwa wanawake ndizo zinachelewesha kuolewa na si kwa sababu hamjapata wananaume sahihi.
Inafika hatua mwanamke kachagua mpaka anakosa hata wa kumchagua matokeo yake anaanza kusema hana mpango wa kuolewa.
Matokeo yake unamkuta mwanamke anawaza kuzaa na mume wa mtu labda kibosile fulani ili aendelee na maisha yake.
Si wote ila baadhi ya wanawake wanafikia hatua hii kwa sababu ya mambo madogo kama niliyoeleza na matokeo yake athari zinakuwa kubwa zaidi ya ambayo angekutana nazo kwa mwanaume ambaye awali aliona si chaguo lake
Tags