Waziri Aliyetangaza Kufunga Mpaka Wa Tanzania Akutwa Na Corona



Waziri wa afya nchini Zambia, Chitalu Chilufya ametangazwa kuambukizwa virusi vya corona ikiwa ni siku chache baada ya waziri wa habari nchini humo kukutwa na virusi hivyo.
Ikumbukwe kuwa waziri wa habari, Dora Siliya alitangaza kuwa amepata virusi hivyo siku kadhaa kabla ya kushiriki kikao cha baraza la mawaziri mjini Lusaka.

Siku kadhaa zilizopita waziri wa afya nchini humo Chitalu Chilufya alitangaza kufungwa kwa mpaka kati ya Zambia na Tanzania ikiwa ni sehemu ya mapambano dhidi ya virusi hivyo.

Mpaka sasa Zambia ina jumla ya wagonjwa 1,057 huku idadi ya waliopona ikifika 779.

Maoni yaliyotolewa katika taarifa hii ni ya mwandishi mwenyewe, hayana uhusiano na Opera News
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad