Waziri Hasunga Amesema Tani 4,000 za Sukari Zimeingia Nchini


Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga amesema sukari tani 4,000 za zimeshaingia nchini.

Amesema tani 21,000 za sukari zitaingia ifikapo mwishoni mwa mwezi na kutatua changamoto ya kukosekana kwa bidhaa hiyo.

Hasunga amesema uwepo wa ugonjwa wa virusi vya corona duniani ni mojawapo ya sababu iliyosababisha kuchelewa kuwasili kwa sukari nchini.

” Sababu iliyokuwa inasababisha uhaba wa sukari nchini ni meli zilizokuwa zimebeba bidhaa hiyo kufaulisha katika meli zingine na kufanya sukari iliyokuwa inafika nchini kutotosheleza mahitaji”

Aidha, amesema Serikali inatarajia kununua tani 300,000 kutoka NFRA ili kukabiliana na ugonjwa wa virusi vya corona

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad