Wema Sepetu amefichua kwa nini hataki kamwe kuwa na ‘beef’ na baby mama wa Diamond Hamisa Mobetto. Hii ni kwa sababu walikuwa marafiki wa dhati tangu utotoni.
Wema alisema kuwa atadumisha uhusiano wake na Hamisa kwa maana wamefahamiana kwa muda mrefu.
‘Muachane na Diamond, ni mtu mkarimu na mzuri.’ Wema Sepetu ajitokeza kumtetea Diamond baada ya kushambuliwa na Zari
Akizungumza mjini Dar Es Salaam, muigizaji huyo alisema kuwa walijuana na Hamisa kabla ya wawili hao kujuana na msanii Diamond.
Wema alisema kwamba wawili hao wamekuwa wandani na kwamba anaheshimu urafiki wao.
“Someone like Hamisa, I knew from long time ago. I knew way before she even met Diamond. I knew from childhood.” Alisema Wema.
Wema pia alisema palikuwepo tofauti baina yao wakati mmoja lakini walitatua tofauti zao.
”We had our issues and we were not okay, but you know life has to move on. I am not with Diamond, she is not with him, so I do not see why we should beef.” Alizungumza.
Wakati Wema alipoulizwa kama mashabiki wake au watu watarajie wawe na uhusiano na Tanasha Donna hakujibu bali alicheka.
Wema alikuwa mpenzi wa kwanza wa Diamond na walichumbiana kwa muda kabla ya kutemana. Uhusiano wao uliwavutia wengi na kuwataka waoane.
Matarajio ya wengi hata hivyo hayakutimizwa kwani Wema na Diamond walitengana.