WHO: Baadhi ya Tiba Zinaashiria Kupunguza Ukali wa COVID-19
0
May 12, 2020
Shirika la afya ulimwenguni WHO linasema hadi sasa, baadhi ya tiba zimeashiria kupunguza ukali au urefu wa ugonjwa wa COVID-19, na kwamba wanazifanyia utafiti zaidi tiba nne au tano ambazo zimeonyesha matumaini, ingawa hakuna tiba iliyopatikana ya kuweza kuzuia au kuua virusi hivyo.
WHO inaongoza mkakati wa kidunia wa kuvumbua chanjo thabiti na salama, majaribio na dawa za kuzuia, upimaji na kutibu maradhi hayo yaliyowaathiri watu zaidi ya milioni 4.1 duniani kote.
Mkurugenzi wa shirika hilo Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema mifumo thabiti ya afya ndio kinga imara sio tu kwa magonjwa ya mlipuko, bali pia vitisho tofauti vya afya vinavyowakabili wananchi kila siku.
Shirika hilo liliashiria hali ya tahadhari kuhusu matarajio ya chanjo, ingawa limesema virusi vya corona kwa ujumla ni aina ya virusi vigumu kuweza kupatiwa chanjo
Tags