Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema dawa inayopulizwa mitaani ktk baadhi ya Nchi kama njia ya kujikinga na corona haisadiii chochote kwenye kuua virusi hivyo>>
”kupuliza dawa mtaani hakuui corona, inaweza kuleta hatari kwa Watu kuugua magonjwa mengine yatokanayo na kuvuta hewa yenye kemikali”
WHO wanakuja na tamko hili zikiwa zimepita takribani siku 25 tangu Rais Magufuli aliposema kuwa upulizaji wa dawa mitaani hauwezi kuua corona, JPM alitoa kauli hiyo akiwa Chato April 22,2020.
Rais Magufuli alisema>>
”DSM, na Mwanza niliona mabasi yanapulizwa dawa na hasa DSM, hakuna upuliziaji dawa unaoweza kuua corona, ingekuwa pakipulizwa corona wanakufa, Nchi zinazoendelea wangemwagia Nchi zao kwa Ndege na wasingekuwa wanakufa, kule kupuliza dawa ni upuuzi tu”