WHO Yakanusha Madai ya Tanzania Kuhusu vifaa vya Kupima Virusi vya Corona
0
May 08, 2020
Shirika la Afa Duniani WHO leo hii limeyakataa madai ya rais wa Tanzania John Magufuli kwamba kumekuwa na kasoro katika vifaa vya kupimia virusi vya corona nchini humo.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Mkurugenzi wa WHO kwa Afrika Matshidiso Moeti amesema hawakubaliani na kile alichokisema rais Magufuli.
Taarifa hiyo inatolewa baada ya Jumapili iliyopita rais huyo wa Tanzania kusema vifaa vya kupima vimekuwa na kasoro, na kubaini kupatikana kwa virusi vya corona katika papai na mbuzi.
Taarifa hiyo inafuatia ile ya awali ya Mkuu wa Kituo cha Udhibiti wa Magonjwa na Kinga barani Afrika CDC, ya Dk. John Nkengasong ambaye alisema Tanzania inatumia vipimo vilivyotolewa na CDC ya Afrika kwa kushirikiana na wakfu wa mfanyabiashara wa kichina Jack Ma Foundation, ambavyo vimetimiza vigezo vya kimataifa.
Katika mkutano wake kwa njia ya simu na waandishi wa habari, mkuu huyo wa CDC barani Afrika anasema kwa wanavyofahamu vifaa hivyo vinavyotumika Tanzania vinafanya kazi vyema kabisa na kwamba yapo mataifa mengine yanatumia vifaa kama hivyo.
Kwa upande wake msemaji wa serikali ya Tanzania amesema serikali imeunda timu ya wataalam, kuchungua maabara hiyo iliyoendesha vipimo na itatoa matokeo yake baada ya uchuguzi kukamilika. Tanzania imethibitisha maambukizo 480 ya virusi vya corona na vifo 18.
Tags