WHO yaonya kuhusu kuharakisha kuondoa vizuwizi


Mkurugenzi mtendaji wa huduma za dharura wa Shirika la Afya Ulimwenguni WHO, Mike Ryan amesema hatari ya kuanza tena mripuko wa virusi vya corona unatatiza juhudi za kuzuwia madhara zaidi kwa mamilioni ya watu ambao wamepoteza kazi, na ameonya kuwa dunia bado imo katikati ya wimbi la kwanza la janga hili. 

Tumo katika awamu ambamo ugonjwa unaongezeka, Ryan amewaambia waandishi habari , akitolea mfano mataifa ya Amerika Kusini, Asia Kusini na maeneo mengine ambayo idadi ya maambukizi bado inapanda. 

Marekani itaanza kupiga marufuku kuanzia leo wageni wanaoingia kutoka Brazil, ambako maambukizi yanaongezeka katika jamii bila kuwapo ishara ya kupungua. 

Marufuku hiyo ambayo ilipangwa kuanza Alhamis, imerudishwa nyuma na itaanza leo, licha ya kuwa hatua hiyo haitawahusu raia wa Marekani wanaoerejea nchini mwao. 


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad