Yericko Nyerere "Chadema Haina Mamlaka ya Kumfuta mtu Ubunge, Bali ila Mamlaka ya Kufuta Uanachama wa Mbunge"


Yericko Nyerere "Chadema Haina Mamlaka ya Kumfuta mtu Ubunge, Bali ila Mamlaka ya Kufuta Uanachama wa Mbunge"
Na Yeriko Nyerere:
Mlio Karibu Na Ndugai Msaidieni Kumuelewesha Asijipotoshe...
Sisi Kama Chama Cha Siasa Hatuna Mamlaka Ya Kumfutia Mtu Ubunge.. Sisi Kama Chama Tumewafutia Uanachama Wabunge Wanne(4) Ambao Tuliwadhamini Mwaka 2015 Ili Kukidhi Matakwa Ya Ibara Ya 67(1)(b) Ya Katiba Ya Tanzania.....

Kwanini Wabunge Hawa Wamefutiwa Uanachama???
Katiba Yetu Imeweka Mwongozo Wa Wabunge Wanaotokana Na CHADEMA. Mwongozo Wa Wabunge Unasema Kwamba;

 Bila Kuathiri Kanuni Na Taratibu Za Bunge Na Maadili Ya Viongozi Na Wanachama Wa CHADEMA Kama Ilivyo Katika Katiba Ya Chama,Wabunge Kwa Tiketi Ya CHADEMA Wanapaswa Wazingatie Masharti Ya Mwongozo Huu Kama Ifuatavyo:

(a) Mbunge Anatakiwa Kutii Na Kutimiza Maagizo Anayopewa Na Chama Kupitia Vikao Halali Na Kama Hakubaliani Na Maagizo Hayo Aeleze Hivyo Kupitia Taratibu Za Ngazi Zilizowekwa Katika Katiba Hii.

(b) Itakuwa Ni Mwiko Kwa Wabunge Kukashifu Chama Ama Kiongozi Wa CHADEMA Ndani Au Nje Ya Bunge

NIDHAMU:
Bila Kuathiri Maadili Na Taratibu Za Kinidhamu Zilizopo Katika Katiba Ya Chama, Makosa Yafuatayo Yatahesabiwa Kama Ni Makosa Ya Kinidhamu Na Yatastahili Adhabu;
(a) Mbunge Kukaidi Maagizo Ya Chama
(b) Mbunge Kukashifu Chama Ndani Au Nje Ya Bunge
(c) Mbunge Kulaumu Au Kulalamikia Maamuzi Ya Vikao Vya Chama Nje Ya Chama...

HATUA ZA KINIDHAMU...
Katiba Yetu Imeeleza Vyema Hatua Za Kinidhamu Kwa Wabunge,Mameya/Manaibu Meya,Wenyeviti Wa Halmashauri,Madiwani, Wenyeviti Wa Vitongoji,Vijiji Na Mitaa Ambao Wametenda Makosa Ya Kinidhamu (Rejea Kipengele i-xi)...
Waliokuwa Wabunge Wa CHADEMA Selasini,Silinde,Komu & Rwakatare Walitumbukia Katika Makosa Ya Kinidhamu..
Sasa, Chama Kimechukua Hatua Za Kinidhamu Dhidi Yao Ya Kuwafutia Uanachama...
Na Kwa Kurejea Katiba Ya Nchi Ibara Ya 71 (1) (e) Inasema..
"Ikiwa Mbunge Ataacha Kuwa Mwanachama Wa Chama Alichokuwamo Wakati Alipochaguliwa Au Alipoteuliwa Kuwa Mbunge".
Sasa, Hao Wabunge Wanne Wamefutiwa Uanachama Wao, Hivyo Automatically Wanapoteza Sifa ya kuwa Wabunge.

Cdm haina mamlaka ya kumfutia mtu ubunge wake kama unavyo dai.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad