Kisukari kinaweza kujijenga pole pole katika mwili wakati mwingine bila hata wewe kufahamu. Ni muhimu kuzitambua dalili za mwanzo ili uweze kuudhibiti kabla haijawa shida
Kukojoa mara kwa mara na kiu iliyozidi kiwango; Kiwango cha juu cha sukari kwenye damu kinazipa kazi za ziada figo na kukusababishia kukojoa mara kwa mara ili kuiondoa sukari iliyozidi mwilini hivyo husababisha kiu
Uchovu usioisha hata baada ya kuwa umepata usingizi mzuri usiku ni kati ya ishara kuu za mwanzo za Kisukari. Kuchelewa kupona vidonda, sukari inapozidi mwilini huishusha kinga ya mwili na mwili kuwa na uwezo mdogo wa kujitibu
Kupungua kwa uwezo wa kuona. Ganzi na miguu kuwaka moto na kuchoma choma. Wanaosumbuliwa na kisukari mara nyingi hupatwa na ganzi. Kupenda vyakula na vinywaji vitamu. Kisukari kinaweza kukuletea hamu au kiu ya kutaka kula au kunywa vitu vitamu vitamu
Ikiwa unatokewa na dalili moja au zaidi kati ya hizi ni vyema kufanya kipimo cha kisukari na kuchukuwa hatua za kujikinga kabla hali haijawa mbaya