Siku ya Ijumaa iliyopita taarifa kubwa ilikuwa ni kutenguliwa kwa uteuzi wa mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo pamoja na Mkurugenzi na mkuu wa Wilaya ya Arusha.
Jumatatu ya jana ikawa ni siku ya kuapishwa mkuu wa Arusha mpya ambaye ni Mh.Iddy Kimanta pamoja na mkurugenzi na mkuu wa Wilaya mpya,
Katika uapisho huo ambao ulifanyika Ikulu jijini Dar Es Salaam Rais Magufuli alieleza sababu za kutengua uteuzi wa viongozi hao ikiwemo baadhi ya migogoro aliyosema ilisababishwa na aliyekuwa mkuu wa mkoa Mrisho Gambo.
Baada ya Uapisho huo Mrisho Gambo alimeandika ujumbe huu:-
Hongera sana Mzee wangu Iddy Kimanta Kwa kuteuliwa na kuapishwa Kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha. Nakutakia kila la heri na Mungu akakusimamie kwenye kazi zako. Rais Magufuli kafanya mambo mengi na makubwa Arusha.