waisraeli wa jadi walichoma bangi ikiwa miongoni mwa tamaduni za kufanya ibada za kidini , utafiti wa matukio ya zamani umebaini.
Mabaki yaliohifadhiwa katika hekalu hilo lenye umri wa miaka 2,700 mjini Tel Arad yametambuliwa kuwa bangi.
Watafiti walibaini kwamba bangi huenda iichomwa ili kuwashawishi waumini.
Huu ni ushahidi wa kwanza wa dawa za kisaikolojia zilizotumiwa katika ibada za zamani za Kiyahudi, kulingana na ripoti ya vyombo vya habari vya Israeli.
Hekalu hilo liligunduliwa mara ya kwanza katika jangwa la Negev yapata kilomita 95 kusini mwa mji wa Tel-Aviv miaka ya 60.
Katika utafiti huo mpya, uliochapishwa katika chuo kikuu jarida la matukio ya zamani katika chuo kikuu cha Tel aviv , watafiti hao wa mambo ya zamani wanasema kwamba madhabahu mawilili yaliojengwa na mawe ya chokaa yalikuwa yamezikwa katika eneo hilo takatifu.
Hali kavu ya hewa na kuzikwa kwa mabaki hayo yalisababisha kuhifadhika juu ya madhabahu hayo.
Ubani ulipatikana katika dhabahu moja , kitu ambacho sio cha kushangaza kwasababu ya umaarufu wake katika maandishi matakatifu , wanzilishi wa utafiti huo waliambia gazeti la Israel la Haaretz.
Hatahivyo, tetrahydrocannabinol (THC), cannabidiol (CBD) na cannabinol (CBN) - viungo vyote vinavyopatikana katika bangi vilipatikana katika dhabahu la pili.
Utafiti huo unaongezea kwamba matokeo ya Tel Arad yanaonesha bangi ilikuwa na jukumu wakati wa ibada katika hekalu la Jerusalem.
Hii ni kwasababu wakati huo eneo hilo takatifu la mjini Arad lilikuwa ngome iliopo mlimani katika mpaka wa kusini wa Ufalme wa Yuda na inadaiwa kufanana na maelezo ya hekalu la kwanza la Jerusalem.
Mabaki hayo ya hekalu mjini Jerusalem sasa yanachunguzwa na wanaakiolojia ili kuwasaidia kuelewa jinsi ibada zilivyofanyika katika hekalu hilo kubwa.