Bayern Munich Hawakamatiki...Washinda taji la Bundesliga Mara Nane Mfululizo

 


Timu ya Bayern Munich imetwaa taji la ligi kuu ya soka Ujerumani Bundesliga kwa mara ya nane mfululizo.

Bayern ilitwaa kombe la msimu huu jana, baada ya kuishinda Werder Bremen bao moja kwa sifuri, bao lililofungwa na Robert Lewandowski katika kipindi cha kwanza.

Ushindi wa Bayern, uliifanya kuwa na pointi 10 mbele ya Borrussia Dortmund wanaoshikilia nafasi ya pili kwenye ligi hiyo.

Na hivyo hata Dortmund wakishinda mechi tatu ambazo wamesalia nazo, bado hawawezi kuipiku Bayern. Mabingwa hao wa Ujerumani Bayern Munich sasa wametwaa ushindi wa ligi hiyo mara 30.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad