Billnass Atoa SIRI Kubwa ya Kumrudia Mwimbaji Nandy "Bugana na Interview ya Millard Ayo ilifanya Jambo"

Billnass anaeleza kwamba penzi lake na Nandy lilivunjika kutokana na kuchukuliana poa kwa sababu yakuzoeana sana, pia utoto. Lakini BUGANA ilirudisha penzi hilo kwa kasi.

Kwenye XXL Clouds FM leo, Nenga amesema wimbo wa BUGANA ndio uliwafanya warudiane

"Bugana ndio ilitufanya turudiane, baada ya kutoka kwenye ile Interview ya Millardayo tulipata comment nyingi sana zikitusifia na kusema tunaendana, ilipelekea hadi kuvunja uhusiano wangu niliokuwa nao. Nikawa single tu. Baadaye tulianza kuwa karibu sana na Nandy na tuliyapitia mapungufu yetu ya awali na hatimaye kuwa pamoja tena." amezungumza Nenga.

Mwezi uliopita Billnass alimvisha Nandy pete ya uchumba na kuchochea kuni za penzi lao.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad