Boniface Jacob "Hivi Karibuni Tundu Lissu Atazungumza na Kueleza Yupo Wapi"


Meya wa Ubungo Boniface Jacob amesema kuwa, huenda siku mbili zijazo aliyewahi kuwa Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu, ataweza kuzungumza na kueleza yuko wapi na anafanya nini.

Meya Jacob ameyabainisha hayo leo Juni 4, 2020, wakati akizungumza na EATV&EA Radio Digital, kufuatia picha aliyoiweka kwenye ukurasa wake wa Twitter siku za hivi karibuni, akiwa amepiga picha na Tundu Lissu na kuandika maneno ya karibu nyumbani.

"Ile picha ni ya siku za hivi karibuni, na mimi nilifanya vile kama kumkaribisha tu arejee nyumbani, lakini kusema yeye yuko wapi na anafanya nini, atazungumza yeye mwenyewe siku mbili zijazo hata usiwe na papara" amesema Meya Jacob.

Tundu Lissu alikuwa nchini Ubelgiji kwa ajili ya matibabu, baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 2017, karibu na makazi yake Jijini Dodoma, na alipelekwa nchini Kenya kwa ajili ya matibabu na hatimaye alisafirishwa hadi nchini Ubelgiji kwa ajili ya matibabu zaidi.
Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Aliyekuwa Meya wa Ubungo Au
    Meya wa Ubungo.??? Tusaidieni kuelewa.

    ReplyDelete
  2. Hivyo, Kila mtu ni msemaji ktk SAKOZ.?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mdau, Hapana. Ni wanaFamilia pekee. hawa wengine, wana washwa
      washwa na kujitia tia tu. Akhera hawapo na Duniani wanatafutwa.

      Tafarani tupu.

      NCCR Oyeee...!!!
      MBatia Safiii.!!

      Delete
  3. Silinde/Komu/ Lihualikali/Selazini/Lwakatare.

    Firimbi yenu y Fauloyumeisikia na Tumeielewa , Asanteni sana.

    Sacoozi ya Familia inaumbuka. Hizi ni baadhi ya akaunti ambazo zimekuwa akichotea Ruzuku na Posho

    NBC Account # 011103007155
    ECOBANK Account# 0020055401089601

    Zingine ziko Ughaibuni ambazo Mabeberu huwa wanamoatioa Huyu Kibaraka akishirikiana na wenzake katika Genge la Uvunjifu wa amani yetu na Usalama wake kiasi kwamba taifa letu lifikie hatima ya kuuzwa.

    Mbongo yuko kazini na Timu yake Mahiri. Huwa hawalazi zege

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad