BREAKING: Orodha Ya Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga Kidato Cha Tano Na Vyuo Vya Kati 2020
0
June 18, 2020
WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI)SELEMANI JAFO amesema jumla ya wanafunzi elfu 73,101 wamechaguliwa kujiunga na kidato cha tano mwaka 2020 na kutakiwa kuripoti Julai 18 ili kuanza masomo Julai 20 mwaka huu.
Waziri JAFO amesema hayoleo ofisini kwake jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema miongoni mwa wanafunzi waliochaguliwa wanafunzi 1,572 wakiwemo wasichana 685 na wavulana 887 wamechaguliwa kujiunga na shule za vipaji maalumu wakiwamo wanafunzi 4 wavulana wenye mahitaji maalum.
Kwa upande wa vyuo waziri JAFO amesema jumla ya wanafunzi elfu 9,264 wakiwemo wasichana 4,314 na wavulana 4,950 wamechaguliwa kujiunga na vyuo vya elimu ya ufundi, vyuo vya afya na vyuo vya ualimu katika ngazi ya stashahada.
Waziri JAFO anatoa agizo kwa wanafunzi kuhakikisha wanaripoti katika kipindi cha wiki mbili tangu tarehe ya kufungua shule.
<<BOFYA HAPA KUTAZAMA MAJINA>>
Tags