Bungara 'Bwege' Ataja Sababu ya Kuikacha CCM Badala yake Akahamia ACT Wazalendo
0
June 15, 2020
Mbunge wa Kilwa Kusini kupitia Chama cha Wananchi CUF, Seleman Bungara amesema hajawahi kufikiria kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa madai kwamba hakitendi haki kwa wananchi hususani wa upinzani.
Amesema hayo mbele mbele ya waandishi wa habari wakati akitangaza uelekeo wake mpya wa kukikahama Chama Cha wananchi CUF na kujiunga na Chama cha ACT-Wazalendo Mara baada ya kuvunjwa rasmi kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Juni 16, 2020.
Aidha Selemani Bungara maarufu kwa jina la 'Bwege' amesema ameamua kuihama CUF kwa kuwa kimeshindwa kuwaunganisha wananchama wake wa Tanzania bara na visiwani na hivyo kupoteza sifa ya kusimamia misingi yake ya mwanzo.
Waswahili wanasema subira yavuta heri, hivi sasa ndio kwanza kila chama ni kama kumekucha, milango ikifunguliwa kwa watu kujitokeza kutangaza nia zao kwenye kuwania nafasi mbali mbali za uongozi kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2020.
Tags