Bunge Lapitisha Bajeti ya Serikali Trilioni 34.88 kwa Mwaka 2020/21


Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Juni 15, 2020, limepitisha rasmi Bajeti ya Serikali ya mwaka wa fedha 2020/21,kiasi cha Trilioni 34.88, kwa kupigiwa kura za NDIYO 304 na kura za HAPANA 63.

Wakati zoezi la upigaji wa kura hizo asilimia kubwa ya Wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), walipiga kura za hapana, ambapo kati ya kura 371, kura 63 zilikuwa za hapana na Wabunge 13 hawakuwepo Bungeni.

Wakati akisoma Bajeti Kuu ya Serikali ya mwaka wa fedha 2020/2021, Juni 11, 2020, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango, alielezea hali ya ukuaji wa Pato la Taifa na kusema kuwa unatarajiwa kupungua kutoka maoteo ya awali ya 6.9% na kufikia 5.5% mwaka 2020, ikilinganishwa na 7% mwaka 2019, hii ni kutokana na mvua nyingi ambazo zimeharibu miundombinu ya usafirishaji nchini na athari ya COVID–19.

Kati ya Bajeti hiyo iliyotengwa na Serikali ya jumla ya Tsh Tril 34.88, kati ya fedha hizo, Tril 22.10 zimetengwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida sawa na asilimia 63 ya bajeti na Tsh Tril 12.78 ni kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad