Chadema "Hatuma Imani na Uchunguzi wa Polisi Kwenye Tukio la Mbowe



Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema hakina imani na uchunguzi unaofanywa na Polisi kuhusiana na tukio la Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe

Kimedai shambulizi la Mbowe linashabihiana na alilofanyiwa Makamu Mwenyekiti Bara, Tundu Lissu, na kwamba tofauti ni kiwango cha madhara

Hivi karibuni Jeshi la Polisi kupitia kwa msemaji wake, David Misime, lilitoa ripoti inayoonesha kuwa Mbowe hakushambuliwa kama inavyodaiwa bali alianguka kutokana na kulewa

Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika, amesema chama kinaendelea kutafakari hatua za ziada za kuchukua na kuutaka umma upuuze njama alizodai zinatumika kuhalalisha kauli za uongo kipindi hiki cha Uchaguzi

Amesema, “Kipimo cha ulevi ni suala la kitabibu, ajitokeze daktari aliyempokea Mbowe na kumpima na Polisi itoe ushahidi wa ‘CCTV’ kuthibitisha madai kwamba alianguka akiwa amelewa.”

Ameongeza, “Tulidhani Polisi itaendesha uchunguzi huu kitaalamu, kauli ya IGP (Mkuu wa Polisi, Simon Sirro) inaashiria bado Jeshi linajihusisha katika propaganda hasi."
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Heeh, Makubwa haya..!!

    Hivyo..!! Hii Saccozi bado ipo Hai.??

    Nnavyo juua Milango ilishafungwa ila
    moja ya locki ilikuwa na kutu.

    Faru joni naona anawachanganyaga..!!

    Mmeshafika kwa Mbungo? mchezo wenu uko
    huko, msibabaishe Mtandaaoni.

    Tuko Mil 60 na tunaimani na vyombo vya
    ulinzi na Usaama vya Taifa.

    Usanii wenu hauna haiba wala Watazamaj

    ReplyDelete
  2. Heeh, Makubwa haya..!!..IMEKULA KWENU

    Hivyo..!! Hii Saccozi bado ipo Hai.??

    Nnavyo jua Mie,Milango ilishafungwa ila moja ya locki ilikuwa na kutu.

    Faru Joni Kiboko kwei, naona anawachanganya..!! Hamjielewi kabisa
    hamjui mshike lipi mwache lipi! TAFARANI tupu. Si mwache siasa Zenu MCHWARA au mnataka tuwasaidie Fikra.

    Mmeshafika kwa Mbungo? mchezo wenu uko
    huko, msibabaishe Mtandaaoni.

    Tuko Mil 60 na tunaimani na vyombo vya
    ulinzi na Usaama vya Taifa.

    Usanii wenu hauna haiba wala Watazamaj

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad