Chadema Mtifuano Mkali....Wafahamu Waliotangaza nia ya Kugombea Urais kwa Tiketi ya CHADEMA Mpaka Hivi Sasa
0
June 15, 2020
Ikiwa ni mwaka wa Uchaguzi kuna viongozi mbalimbali waliotangaza nia ya kuwania Urais Chadema lakini kwenye vyama vingine wakifungua milango, Siku ya jana Mbunge wa Iringa Mjini kupitia CHADEMA, Mchungaji Peter Msigwa ametangaza rasmi nia yake ya kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa 2020.
Amesema kuwa:-
“Kama nilivyotangaza siku chache zilizopita, leo natangaza rasmi nia yangu ya kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa mujibu wa sheria na taratibu za CHADEMA tayari nimewasilisha taarifa rasmi ya nia yangu ya kugombea“, amesema Msigwa.
“Kwanini ninautaka Urais?, nataka kuongoza mageuzi makubwa ya kiutawala, kiuchumi na kielimu yatakayoleta maendeleo makubwa na ya haraka na endelevu kwa manufaa ya sasa na Tanzania ijayo“, ameongeza Msigwa.
Pia Msigwa amesema kuwa Bado Tanzania ni moja ya nchi masikini zaidi duniani ambapo kwa mujibu wake, uchambuzi wa Benki ya Dunia kuhusu mapato na matumizi ya kaya mwaka 2018 umeonesha zaidi ya nusu ya Watanzania wanaishi katika umasikini wa chini ya Dola 1.90 kwa mtu mmoja kwa siku.
Kuhusu vipaumbele atakavyovisimamia, Msigwa amesema, “endapo nitapata heshima na dhamana ya kuongoza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, nitajikitia kwenye vipaumbele vikuu vitatu, kufanya mageuzi ya kielimu, kujenga utawala wa uwajibikaji na kufanya mageuzi makubwa ya kuichumi“.
Peter Msigwa na Tundu Lissu na Lazaro Nyalandu ndiyo viongozi wa chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA waliotangaza rasmi nia ya kugombea Urais mpaka sasa kwenye chama hicho na kuwasilisha taarifa rasmi kwa uongozi.
Kauli ya Nyalandu ni kwamba “Endapo chama changu kitaniteua kugombea na Watanzania wakanipa ridhaa ya kuwaongoza, nitasimamia mambo yafuatayo nadi ya siku 100. Kwanza nitaunda maridhiano ya kitaifa, ili kuwaunganisha watu wote, Jambo la pili, ndani ya siku 100, tutaandaa mpango wa kufuta sheria zote kandamizi zinazosababisha watu kuwekwa kizuizini bila kupewa dhamana kisha tutawatoa gerezani watu wote ambao wamewekwa bila ya kuwepo kwa due process, “Pia nitaongeza ajira kwa vijana na jambo lingine ndani ya siku 100 nitaanza upya mchakato wa mapitio ya Katiba Mpya kuanzia ile ya Jaji Warioba. Jambo la sita tutairekebisha TRA ili iwe ni taasisi isiyolalamikiwa kwa namna yoyote ile”
Kwa Upande wa Tundu Lissu alisema kuwa:-
”Nina wajibu wa kutaja kile kilichonisukuma kutaka kugombea nafasi hii ya juu kabisa kiungozi katika mfumo wa kikatiba wa nchi yetu yaani Rais wa Jamuhuri ya Muungano ,”Amesema Lissu
”Kwa kipindi cha miaka mitano itakayoishia Oktoba mwaka huu nchi yetu imetawaliwa na serikali ya Rais John Pombe Magufuli na Chama cha Mapinduzi , CCM kwa namna ambayo imeiweka nchi yetu katika mtihani mkubwa kiuchumi, kisiasa na kidiplomasia.Kwa mtihani huu nchi yetu iko njia panda, na kwa vyovyote vile itakavyokuwa uchaguzi wa mwaka huu utakuwa na umuhimu mkubwa katika historia ya nchi yetu”.
Tags